๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ Mchezo wa maisha ya Dar es Salaam

Ishi maisha yako ya Dar โ€” na watu halisi.

Tafuta kazi, kula chipsi mayai, kula bata Sinza, endesha bodaboda, nunua kiwanja Kigamboni na uwe Mkuu wa Mkoa. Bure kwenye simu yako โ€” hakuna kudownload.

Bongo Life โ€” mtaa wa Kariakoo
Tengeneza Sim wako
๐Ÿ๏ธ Bodaboda imenunuliwa!
๐Ÿ’ฐ +TSh 24,000 shifti imeisha
๐Ÿงบ Kariakoo๐Ÿข Posta๐Ÿชฉ Sinza๐Ÿฆž Masaki๐Ÿ–๏ธ Coco Beach๐ŸŒด Kigamboniโ›ด๏ธ Kivukoni Feri๐Ÿ›’ Mlimani City๐ŸŸ๏ธ Uwanja wa Taifa๐ŸšŒ Ubungo๐ŸŽ“ UDSMโœˆ๏ธ JNIA inakuja

Kila kitu cha mtaani, kiganjani mwako

Dar es Salaam nzima imejengwa upya โ€” kuanzia Kariakoo mpaka fukwe za Kigamboni.

๐Ÿ’ผ

Chakarika

Kazi 16 โ€” machinga Kariakoo, konda wa daladala, DJ, mvuvi, teller wa benki mpaka developer. Fanya shifti, pandishwa cheo, mshahara upande.

๐Ÿ›

Ishi

Njaa, nguvu, raha, usafi na jamii. Kula kwa Mama Ntilie, ogelea Coco Beach, lala chumbani kwako Manzese.

๐Ÿชฉ

Kula bata

Cheza Club Mzuka, nunua mzunguko kwa washkaji, tazama dabi ya Simba vs Yanga na rekodi ngoma yako studio.

๐Ÿ๏ธ

Endesha

Baiskeli, bodaboda, bajaji, IST, Noah, Harrier mpaka V8. Au panda daladala na bajaji kuzunguka mji.

๐Ÿก

Miliki

Nunua viwanja Kigamboni, Masaki na Mbezi. Jenga villa au ghorofa la kupangisha. Miliki bar, genge au club upate mapato kila saa.

๐Ÿ“ฑ

Simu yako

Chat ya mtaa, meseji za faragha, Bongo Pesa, ramani ya Dar na matangazo โ€” vyote ndani ya simu ya mchezo.

๐Ÿ‘—

Pendeza

Kitenge, kanga, buibui, kanzu, shuka la Kimasai, suti ya Kaunda na jezi za Simba na Yanga.

๐Ÿ‘‘

Tawala

Tajiri namba moja wa Dar anakuwa Mkuu wa Mkoa โ€” jina lake linaonekana kwa kila mtu anayeingia.

Club Mzuka

Gusa jengo, ishi maisha

Kila sehemu ina shughuli zake: ingia club ucheze, nunua meza ya VIP, au anza shifti kama DJ. Kila kitu kinabadilisha njaa, nguvu na raha yako โ€” na mfuko wako.

Simu ya mchezo

Washkaji halisi, kila mahali

Kila mtu unayemwona mtaani ni mchezaji halisi. Piga stori kwenye chat ya mtaa, tuma DM, mtumie mshkaji pesa, au tangaza biashara yako kwenye mabango ya mji.

Anza ndani ya dakika moja

  1. 1

    Jisajili bure

    Jina, username na password tu. Lazima uwe na miaka 18+.

  2. 2

    Tengeneza Sim wako

    Chagua mwili, nywele, mavazi, tabia na mtaa unaoanzia.

  3. 3

    Ingia mtaani

    Unaanza na TSh 50,000 mfukoni na chumba Manzese. Mengine ni juu yako.

Ongeza salio kwa M-Pesa

Unataka kununua V8 haraka? Ongeza salio la mchezo kwa M-Pesa, Mixx by Yas au Airtel Money โ€” sekunde chache tu. Si lazima: unaweza kufika juu kwa kuchakarika tu.

Pesa ya mchezo ni ya burudani tu: haiwezi kutolewa wala kubadilishwa kuwa pesa taslimu.

M-PesaMixx by YasAirtel MoneyHaloPesa
๐Ÿ“ข Kwa biashara

Tangaza kwa Wabongo wanaocheza kila siku

Mabango 11 katikati ya mji โ€” Posta, Kariakoo, Coco Beach, Masaki na Daraja la Nyerere. Weka picha, ujumbe na link ya biashara yako moja kwa moja ndani ya mchezo kupitia Simu โ†’ Matangazo.

Tangaza Hapa!๐Ÿ“ข Posta CBD

Maswali ya mara kwa mara

Je, ni bure?

Ndiyo. Kujisajili na kucheza ni bure. Kuongeza salio ni hiari kabisa.

Nahitaji kudownload app?

Hapana. Bongo Life inafunguka moja kwa moja kwenye browser ya simu (Chrome au Safari). Unaweza kuiweka kwenye home screen kama app.

Inafanya kazi kwenye simu yangu?

Simu nyingi za Android na iPhone za miaka ya karibuni zinaweza. Kama inakwama, chagua Graphics โ†’ Chini kwenye Mipangilio.

Naweza kutoa pesa ya mchezo?

Hapana. TSh za ndani ya mchezo ni za burudani tu โ€” haziwezi kutolewa, kuuzwa wala kubadilishwa kuwa pesa halisi.

Ni kwa umri gani?

Bongo Life ni kwa watu wenye miaka 18 na kuendelea.

Ni kwa Kiswahili au Kiingereza?

Vyote viwili. Badilisha lugha muda wowote kwa kitufe cha ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ/๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ง.

Mtaa unakusubiri.

Jiunge na Wabongo wanaoishi maisha yao ya Dar sasa hivi.

Cheza bure sasa โ†’